Posts

Rais Magufuli ateta na Balozi mpya wa Marekani

Image
MWANDISHI WETU– DAR ES SALAAM RAIS Dk. John Magufuli amesema Tanzania itaendeleza uhusiano wake mzuri na kati nchi za Marekani na Vietnam Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Dar es Salaam jana, ilisema Rais Dk. Magufuli alipokea hati za utambulisho za mabalozi wawili walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa Tanzania. Waliowasilisha hati hizo Ikulu, Dar es Salaam ni Dk. Donald Wright aliyeteuliwa kuwa Balozi wa Marekani hapa nchini na Nguyen Nam Tien, aliyeteuliwa kuwa Balozi wa Vietnam hapa nchini. Katika mazungumzo baada ya kupokea hati hizo, Rais Magufuli amewakaribisha mabalozi hao na ameeleza kuwa Tanzania itaendeleza na kukuza zaidi uhusiano mzuri na wa kihistoria uliopo kati yake na nchi hizo. Mhe. Rais Magufuli amewaomba Mabalozi hao kuwahamasisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchini mwao kuja kuwekeza hapa nchini na kwamba Serikali itakuwa tayari wakati wowote kutoa ushirikiano kwao. Akizungumza baada ya kuwasilisha hati zake za u...